Mwalimu: Alwiya Omar
648 Williams Hall
Simu: 898 4299
Lengo la darasa:
Kuimarisha ujuzi wa kuzungumza, kusikiliza, kusoma, na kuandika
Kuimarisha kusikiliza:
a. Kusikiliza taarifa za habari kutoka idhaa za Kiswahili za: Sauti ya
Amerika, Sauti
ya Ujerumani, na Sauti ya
Kenya.
b. Kusikiliza kanda za Kiswahili: Kanda za video kutoka vipindi vya
televisheni vya Tanzania
Darasani, wanafunzi watafanya majadiliano juu ya habari mbali mbali na
maelezo kutoka kanda
Kuimarisha kuzungumza
a. Kila siku ya darasa, kila mwanafunzi azungumze kuhusu jambo au
habari fulani na wanafunzi wengine wasikilize na waulize maswali.
b. Kuzungumza kuhusu mradi wa darasa (class project)
c. Kushiriki katika mazungumzo ya Kiswahili
d. Kushiriki katika siku ya utamaduni wa lugha za Kiafrika
Kuimarisha kusoma na kuandika
a. kuandika insha na kuziweka katika ukurasa wa web.
b. Kusoma habari za magazeti na kuandika muhtasari.
c. Kusoma kitabu cha Kuli kilochoandikwa na Adam Shafi na kufanya mazoezi
ya kuandika na kuzungumza.
Kufundisha darasa la kwanza la Kiswahili
Kila mwanafunzi atayarishe kufundisha darasa la mwaka wa kwanza wiki mara
moja kwa muda wa dakika 30.
Mtihani
Kutakuwa na mtihani wa mwisho ambao utakuwa na sehemu mbili: 1) Kusoma na
kuandika na 2) kuzungumza
Rudi ukurasa mkuu wa Kiswahili
For more
information, please contact:
African
Studies
Center
642 Williams Hall
Unversity of Pennsylvania
Philadelphia, PA 19104
Tel: 215 898 6971
Last Modified: March 31st, 1998
Alwiya
S. Omar, asomar@babel.ling.upenn.edu
African Language Coordinator