Jarida la Wanafunzi wa Kiswahili
|
Toleo la pili (Fall 97). Someni kwa furaha!
==========================================================
K W A N Z A A
na Tonyardzwa Taylor, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Kwanzaa Yenu Iwe Na Heri!
Kwanzaa ni sherehe ya "African-Americans". Tunashangilia uhai
Dr. Maulana Karenga, mwalimu mkuu za historia "African-American" katika
chuo kikuu cha California alianzisha Kwanzaa mwaka 1966. Kwanzaa
inasherehekewa kwa muda waa siku saba, kutoka Desemba ishirini na sita
mpaka Januari moja, kwa kufuata nguzo saba. Nguzo hizi saba ni:
1. Umoja (Unity)
2. Kujichagulia (self-determination)
3. Ujima (collective work and responsibility)
4. Ujamaa (cooperative economies)
5. Nia (purpose)
6. Kuumba (creativity)
7. Imani(faith)
Pia kuna alama saba:
1. Kikombe cha Umoja (Unity cup): Tunakunywa kutoka kikombe cha umoja
2. Kinara (candle holder): Kinara kinashika mishumaa
3. Mazao (fruit)
4. Mkeka (straw mat)
5. Mishumaa Saba (seven candles)
mishumaa mitatu ina rangi kijani yenye Maana ya matumaini
mishumaa mitatu ina rangi nyekundu yeny maana ya kupigania uhuru
mshumaa mmoja una rangi nyeusi yenye maana ya umoja wa watu weusi
6. Mahindi (ears of corn) ni dalili ya watoto na maendeleo
7. Zawadi(gifts)
Unaweka Kinara juu ya Mkeka. Mishumaa saba inafanana na nguzo saba.
Unawasha mshumaa mmoja kila siku.
Unaanza kwa mshumaa mweusi. Siku ya pili unawasha mshumaa wa kushoto, siku
ya tatu unawasha mshumaa wa kuume.
Chakula cha sherehe ya Kwanzaa, jina lake ni Karamu. Kwa kawiada inaanza
tarehe thelathini na moja Desemba. Jamaa wanasimulia nguzo ya siku na
wanatoa mawazo yao juu ya nguzo hii. Baada ya kuwasha mishumaa, jamaa
wanafanya
ukumbusho wa watu wa kale. Wanankuywa kutoka kikombe cha Umoja. Baada ya
kunywa, wanainua juu kikombe cha umoja na wanasema "harambee". Maana ya
ÒharambeeÓ ni "let's pull together". Tunakula viazi vitamu, mchuzi wa
mboga, keki za kunde, na mabamia ya kukaanga.
*************************************
BENDERA ZA AFRIKA
na Noelle Lee (Mwihaki), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Katika Afrika kuna bendera hamsini na tatu; bendera moja kwa
kwa kila nchi ya Afrika. Bendera za Afrika zina rangi ya
kijani, na rangi nyekundu, na rangi ya
manjano. Rangi nyeupe na rangi nyeusi zinatumia sana pia. Alama za nyota
na
mwezi zina maana maalum. Mistari inatumiwa sana pia.
Bendera ya Uganda ina rangi nne: rangi nyeusi na rangi nyeupe, na
rangi ya manjano na rangi nyekundu. Ina mistari ya
rangi nyeusi na rangi nyekundu na rangi ya manjano. Ina duara la rangi
nyeupe na ndege wa rangi nyekundu na rangi nyeupe.
Bendera ya Libia ni rangi ya kijani.
Rangi za bendera ya visiwa vya Comoro ni kijani na kuna nyota nne na mwezi
wa rangi nyeupe.
Bendera ya Tanzania ina rangi nne: rangi ya buluu, rangi ya manjano,
rangi nyeusi, na rangi ya kijani.
Bendera ya Algeria ina rangi mbili - rangi nyekundu na nyota na mwezi wa
rangi nyeupe.
Kwa kawaida, rangi za bendera zina maana maalum. Rangi ya
buluu, kwa mfano, ina maana ya maji. Nyeusi ni rangi ya watu, na ina
maana ya nguvu za taifa. Rangi ya manjano ina maana ya madini au, hasa,
dhahabu. Mara kwa mara, silaha ni alama ya nguvu na uhuru. Ninafikiri
ndege ni alama ya uhuru pia.
Bendera ya Liberia na bendera ya Afrika ya kusini ni tofauti na bendera
nyingine. Bendera ya Liberia ina rangi nyekundu na rangi nyeupe
na rangi ya buluu. Rangi sawa na bendera ya Amerika. Bendera ya Liberia
ina mistari ya rangi nyeupe sita na rangi nyekundu tano. Bendera ya
Amerika ina mistari ya rangi nyeupe sita na mistari wa rangi nyekundu
saba. Bendera ya Amerika ina nyota hamsini lakini bendera ya Liberia ina
nyota moja. Bendera ya zamani ya Afrika ya kusini ni kama bendera ya
Ufaransa na Uingereza.
************************************
KUSOMA KISWAHILI TANZANIA
na Stacey Langwick, mwanafunzi aliyeendelea
Kijifunza Kiswahili katika chuo kikuu cha Pennsylvania ni vizuri,
lakini kusoma kisawili katika Tanzania ni vizuri zaidi. Kiangazi
hiki nilienda Tanzania pamoja na Group Project Abroad Program
inayofundisha na chuo kikuu cha Yale. Darasa hilo linafundishwa
kila mwaka kwa wiki nane tu, lakini wanafunzi hujifunza mambo
mengi. Wanafunzi wote ambao husoma katika darasa hilo walisoma
Kiswahili kwa muda wa miaka miwili au mitatu kabla ya kushiriki
katika programu hii.
Mwaka huu, darasa la Kiswahili lilifundishwa katika Arusha na
Unguja. Katika Arusha, walimu wanne wanaotoka Dar es Salaam
walikuja kufundisha wanafunzi kumi na mbili. Katika Unguja,
wanafunzi hao walifundishwa na walimu wanaofanya kazi Tasisi ya
Kiswahili na lugha za kigeni. Kulikuwa na walimu wengi kwa
wanafunzi wachache tu. Kwa sababu hii, kila mwanafunzi alipata
msaada wa kutosha. Mazingira hayo ni mazuri kusoma lugha mpya.
Pia, wanafunzi walisoma Kiswahili katika darasa kwa muda wa saa tano
kila siku. Baada ya kusoma Kiswahili, wanafunzi walihitaji kusema
Kiswahili katika mji. Kama wakitaka kununua stampu au kadi au
kinywaji, wanahitaji kusema Kiswahili. Kwa wiki nne katika Arusha,
kila mwanafunzi alikaa pamoja na jamaa inayotoka Kimondolo, kijiji
karibu na Arusha. Ninafikiri kwamba kukaa mahale ambapo unahitaji
kusema Kiswahili wakati wote ni njia nzuri zaidi ya kujifunza
Kiswahili kuliko njia nyingine yoyote.
Sehemu mbili bora za darasa hilo zilikuwa kukaapamoja na jamaa
karibu na Arusha na kufanya utafiti kuhusu utamaduni katika Unguja.
Nilipenda kukaa na jamaa inayoishi Kimandolo kwa sababu niliweza
kuzungumza kuhusu vitu muhimu kwa watu wanaoishi Tanzania; niliweza
kusikiliza watu wengi wanaosema Kiswahili; na niliweza kuuliza
maswali mengi. Kwa mfano, nilizungumza kuhusu dawa ya kinyeji na
babu anayeishi ndani ya nymba ambayo nilikaa. Pia, nilizungumza na
mama kuhusu biashara na baba kuhusu siasa. Nilizungumza na mama
mdogo kuhusu mambo mengi kutoka uzazi wa mpango mpaka mapishi.
Nilisomia hadithi mtoto mdogo na watoto wakubwa walinisaidia kazi
yangu ya nyumbani. Katika mazingira haya nilijifunza Kiwahili
kingi, pia nilianza kujifunza kuhusu njia kusema vitu fulani na
wakati gani ulikuwa nzuri wakusema vitu hivyo.
Pili, katika Unguja nilifanya utafiti kuhusu chakula cha Kisiwa cha
Unguja. Nilianza kuandika kitabu cha mapishi katika Kiswahili.
Nilichagua utafiti huu kwa sababu nilitaka kuzungumza na wanawake.
Kwa kawaida, wanawake wanaoishi Unguja hawaendi pahale ambapo
wageni wanawezi kuona kwa urahisi. Wanawake na wanaume wana kazi
tofauti. Wanawake wanatumia muda mingi zaidi wa familia. Kwa
hivyo, nilianza kufanya utafiti wangu pamoja na mama aliyekuwa na
duka dogo nyumbani kwake. Kwanza, nilienda dukani kwake. Nilikaana
nilizungumza na mama na jamaa yake na rafiki zake. Tulizungumza
vitu vingi. Nilkwenda dukani kila siku. Baada ya siku chache, mama
alinikaribisha jikoni kupika vyakula pamoja na familia yake. Pia,
nilisema na wanawake wengine niliokutana nao kuhusu mapishi.
Vilevile, kila jioni nilienda Darajani, kwenye bustani karibu na bandari
ambapo wanaume na vijana wanakuja kupika na kuuza vyakula tofauti
vya Unguja (kama kababu, pwezi, chapati, katlesi, na sambusa) na
vinywaji tofauti (kama maji ya mua na chai ya mchaichai). Watu
wengi -- wazanzibari na wageni, wanawake na wanaume, watoto na watu
wazima -- huenda Darajani kila jioni kula na kukaa karibu na maji.
Mahale bora kujifunza Kiswahili ni Tanzania. Kama ukisoma Kiswahili
kwa miaka miwili au mitatu, unaweza kuandika maombi kuenda Tanzania
pamoja na chuo kikuu cha Yale. Baada ya kurudi, utajua zaidi kuhusu
Kiswahili, kuhusu utamaduni wa waswahili, na kuhusu mazingira ya
uswahili.
**************************************
MCHEZO WA MANENO:
Maneno gani yenye herufi nne au zaidi unaweza kuyatoa kwenye neno
KISWAHILI?
Maneno : akili, asili, hila, hili, hiki, hisi, hisa, haki, hali, halii,
halisi, hawi, hiliki, hawahi, iliki, kiasi, kasi, kali, kaki, kila, kisa,
kili, kisiwa, kiwili, liwa, lisha, lasi, laki, likisha, lia, sali, sala,
sili, siki, sikia, siwi, siwahi, swali, shika, wahi, wali, wakili, wasili,
wiki.
Je, kuna maneno mengine? Niandikie.
*************************************
Toleo la
kwanza
Wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vingine wanaweza kumletea mhariri asomar@ccat.sas.upenn.edu makala mbali mbali
ili zichapishwe
katika toleo la tatu mwezi wa Mei, 1998
Rudi ukurasa mkuu
wa Kiswahili
*************************************
Last Modified: Machi 16, 1998