Jarida la Wanafunzi wa Kiswahili

      Toleo la tatu (Fall 98). Someni kwa furaha!

      ==========================================================

      Wanafunzi wa mwaka wa kwanza

      Kupiga Picha

      Tanji Gillian

      Mimi ninapenda kupiga picha na mimi ninapenda watoto pia. Kwa hivyo, daima ninapiga picha za watoto. Mimi nilisoma sanaa katika chuo kwa miaka miwili. Nilipiga picha katika rangi nyeusi na nyeupe tu. Nilipenda kutembea katika mji wa Willingboro na kupiga picha za watoto wageni lakini mimi nilipiga picha za dada, kaka na mafiki pia.

      Msichana huyu anakaa katika Willingboro. Tunakaa njia moja. Nilipenda kupiga picha za msichana kwa sababu alinitazama mimi.

      Mtoto wa kiume kwa upande mwingine hakunitazama mimi. Mtoto huyu ni kakaangu. Nilimpiga picha penye nyumba ya mama mdogo. Kwasababu hapendi kupiga picha na mimi.

      Wavulana hawa ni majirani zangu. Mimi niliwajua wao tangu walipozaliwa.

      Mwishowe, msichana huyu ni Lucille. Alienda shuleni kwangu. Alikuwa dadaangu katika programu ya kaka mkubwa na dada mkubwa.

      na Tonyardzwa Taylor, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza

      Wanafunzi wa mwaka wa pili

      Mchezo wa 'Volleyball'

      na Kristine S. Stine

      Nilianza kucheza mchezo wa volleybali wakati nilipokuwa miaka kumi na moja. Katika shule ya msingi ambayo mimi nilikwenda watoto wa kike wote walifundishwa kucheza mpira wa volleybali. Wakati nilipokuwa miaka kumi na moja, timu yangu ilishinda mashindano ya kila mwezi katika California ya kusini. Wakati wa nilipokuwa miaka kumi na tatu, nilianza kucheza volleybali katika chama cha mchezo wa volleyball.

      Msimu wa volleybal wa chama ni mwezi wa Desemba mpaka Julai. Kuna watu kumi katika kila timu na kuna timu tatu za wachezaji umri tofauti. Katika chama cha volleybali, tunacheza na timu kutoka pwani magharibi, pamoja na timu kutoka Hawaii. Kuna mashindano ya mwezi karibu kila wikendi. Mashindano ya mwezi yanafanywa katika Los Angeles. Mashindano ya mwezi ni siku moja au mbili katika Los Angeles. Los Angeles iko muda wa saa mbili kwa kuendesha kaskazini ya San Diego. Kwa hivyo, mimi nilicheza volleybali kutoka darasa la saba mpaka kumi na mbili. Katika kiangazi, kwa kawaida ninashiriki katika kambi za volleybali. Baada ya kuhitimu kutoka shule ya sekondari ninaendela kucheza wa volleybali katika koleji. Msimu wa volleybali ni mwezi wa agosti mpaka mwezi wa novemba. Pia, kuna msimu katika "spring", lakini msimu huu unadumu mwezi mmoja na nusu na mashindano. Kwa kawaida, tunacheza michezo miwili kwa wiki. Ikiwa mchezao uko mahali pengine, tunasafiri kwa basi. Mbali zaidi tunaendesha gari.

      Volleybali ni kizuizi juu ya kazi ya nyumbani na maisha ya urafiki. Ninacheza volleybali kwa miaka mitatu katika chuo kikuu cha Pennsylvania na ninaamua sitacheza volleybali mwaka ujayo ili nikaze macho katika kazi ya shule na marafiki zangu.

      *************************************

      MCHEZO WA MANENO:

      Maneno gani yenye herufi nne au zaidi unaweza kuyatoa kwenye neno KUJICHAGULIA?

      Niandikie.

      *************************************
      Toleo la kwanza

      Toleo la pili

      Wanafunzi wa Kiswahili wa vyuo vingine wanaweza kumletea mhariri asomar@ccat.sas.upenn.edu makala mbali mbali ili zichapishwe katika toleo la nne mwezi wa Mei, 1999

      Rudi ukurasa mkuu wa Kiswahili

      *************************************

      Last Modified: December 15, 1998
      Alwiya S. Omar, asomar@babel.ling.upenn.edu
      African Language Coordinator