na Marton Markovits (Salim), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Nilisafiri jimbo la Florida pamoja na mke wangu na Baba na Mama yake mwezi
wa Februari. Annie na mimi tulikwenda kwa ndege Alhamisi, Februari kumi
na nane. Tulikwenda kwa sababu tulitaka kumshangaza Baba mkwe wangu kwa
siku yake ya kuzaliwa. Alitimia miaka sabini.
Tulikwenda bustani ya Disney kila siku wakati tulipokuwa katika
Florida. Siku ya kwanza tulikwenda ÒMagic KingdomÓ. Kule tuliangalia
nyumba ya Mickey Mouse, maandamano ya watu wa Filamu ya Disney na
tulipanda Michezo mingi ya kuzunguka. Katika picha ya tatu Annie anapiga
picha Mama mkwe wangu na mimi wakati tunazungumza kuhusu ÒSpace Mountain.Ó
Siku hii ni nzuri na tulikuwa na wakati mzuri.
Siku ya pili na ya tatu tulikwenda bustani ya Epcot. Tulitembea
sana na tuliangalia sehemu za nchi mbalimbali ambazo zinazunguka ziwa.
Baada ya kutembea sana tulikuwa na njaa sana, tulichoka na kulikuwa na
baridi nje, kwa hivyo tulikwenda kula katika hoteli ya Kitaliana. Chakula
huko ni kizuri na kingi na tulikuwa na furaha usiku huu.
Siku ya tatu tulirudi bustani ya Epcot kuwanunulia zawadi rafiki
yetu. Siku hii ilikuwa na baridi sana na ilinyesha kidogo. Baba mkwe
wangu na mimi tulikuwa wagonjwa pia. Nilikuwa na homa kidogo na niliumwa
na koo, kwa hivyo tulirudi Hotelini kwetu kupumzika kidogo. Huko tulilala
kidogo na tuliangalia televisheni huku Annie na Mama yake walikwenda
madukani.
Ijapokuwa hatukutaka kuondoka ilikuwa Likizo nzuri!
*************************************
Ngoma ya Steel Pan (sufuria)
na Alana Rose (Zahara), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
NIlicheza ngoma ya Trinidad ambayo jina lake ni "steel pan" kwa kingereza,
shuleni kwangu. Nilicheza ngoma kwa miaka miwili. Kundi zetu ilikuwa na
wachezaji kumi na mbili na sufuria sita tofauti. Watu wengi tulipenda
kucheza ngoma lakini sufuria ni ghali na shule yangu tu ilikuwa na kumi na
mbili. Mwanaume alizifanya sufuria zetu. Alitoka Trinidad na anakaa
Boston. Sufuria zifanana debe la taka lakini muziki ni mzuri. Zikumbusha
watu wengi wa "carribbean".
Ninapenda kucheza sufuria yangu. Ni vitu vichache ambayo
ninapenda
kufanya zaidi ya kucheza ngoma. Marafiki zangu wanacheza ngoma pia, na
mazoezi yetu ni sehemu bora ya siku. Tulicheza masaa manne kwa siku ya
wiki kwasababu wachezaji wote walicheza michezo pia. Lakini kwa kawaida
wachezaji wali chukua ngoma nyumbani kucheza. Walisikiliza muziki wa
ngoma
ya Trinidad sana kabla ya kucheza. Katika kundi letu walikuwa na ngoma ya
Afrika pia namna ya njembe. Kundi letu tulisafiri sana. Tulisafiri
Massechusetts na New Hampshire sana na sehemu zote za Maine. Ngoma yetu
ilikwenda kwa motokaa moja na wachezaji walikwenda kwa nyengine.
Tulihifadhi. Ngoma yangu jina lake ni "tenor" na ina thelathini sauti
tofauti . Ngoma yangu ilifanya zamuzik za juu. Ngoma jina lake ni "Bass"
ilifanya zamuzik za cheni. Nyngine ngoma lifanya sauti katikati.
************************************
Kitabu 'Afrika nyengine'
na Aviah Cohen (Dalila), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Kitabu hiki jina lake ni Afrika Nyengine. Katika kitabu
hiki kuna picha na tenzi za Afrika. Robert Lyons alipiga picha na Chinua
Achebe aliandika tenzi. Chinua Achebe ni mwandishi mashuhuri. Anatoka
Nigeria lakini anakaa Marekani sasa. Achebe ni mwalimu katika chuo kiku
cha Bard. Ameandika vitabu vingi kama hivi Things Fall Apart na No
Longer At Ease. Anaandika juu ya jamii kwa Afrika ambazo zina
matatizo kwa Wazungu. Achebe na Lyons wamefanya kazi sana kujitahidi
kitabu hiki amacho ni cha pekee.
Robert Lyons alipiga picha vya vitu tofauti katika Afrika.
Afrika Nyengine ni kitabu ambacho kinaonyesha tofauti mahali ya Afrika.
Katika kitabu hiki kuna picha za jangwa, bahari na majani. Picha hii ni
jangwa ya Mali. Picha hii ni majani ya Uganda.
Picha hii ni bahari ya Zanzibar. Katika kitabu hiki kuna picha za watu
na picha za wanyama. Katika picha hii watu wanapumzika. Katika picha hii
mwanamume anafanya kazi sana katika Mali. Katika picha hii watu wamevaa
mavazi ya kienyeji. Katika picha hii mwanamke hajavai mavazi ya
kienyeji. Amevaa nguo kama hapa.
Picha zote katika kitabu hiki ni nzuri. Tenzi ni nzuri pia.
Afrika ni bara mkubwa ambalo lina makabila mengi. Afrika Nyengine
kijaribu kunaonyesha tofauti vitu.
**************************************
Likizo ya Kiangazi
na Miriam Ackerman (Lela), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Wakati wa likizo yangu ya kiangazi, katikati ya mwaka wa pili wa shule ya
sekondari na mwaka wangu wa tatu, nilisafiri Barbados. Barbados ni kisiwa
katika bahari kuu Atlantika. Nilizuru Barbados kwa mwezi mmoja [Julai
elfu mojia mia tisa tisiini na sita (1996)]. Nilikewnda na wanafunzi
wengine. Tulisafiri Barbados kwa ndege. Tulifanya “kazi ya jamii” katika
Barbados. Tulikaa nyumbani katika shule ya watu ambo hawana akili nzuri.
Pale, tulimfundisha, tuliyapaka manyumba, na tulipika. Kutumia maembe na
sukari, au thumu, wanafunzi wa skuli walipika michuzi, 'jam' na 'chutney'
kuuza. Nilimsaidia kupika; nilimenya thomu. Pia, nilifanya kazi katiki
hoteli na hospitali ya watoto. Hospitalini, nilimsema watoto. Tulicheza
mchezo wa “video” jina lake ni 'Brick' na michezo ya kadi, na michezo ya
maneno, kama “hangman.” Hotelini, rafiki yangu na mimi, tulizikosha
meza. Tulikula sana, pia! Kwa kuwa hoteli ni kando bahari, wanaogeleaji
na wanamaji walikula katika hoteli. Pindi hatukufanya kazi, tulikula,
tulikwenda ufukoni na tuliogelea, na tulisafiri kisiwani. Usiku,
tuliangalia telivisheni nyumbani au tulikwenda kucheza dansa katika mji.
Nilifurahia Barbados, Barbados ni nzuri, lakini sikufurahia watoto wengine
ambawo pamoja na nilisafiri. Kama mtaaenda Barbados, natumai hamtaenda na
watoto kama watoto ambao nilwkenda nao!
Mwinyi, mchezaji wa Baseball
na Chris Clemons, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Wakati wa miezi ya Machi, Aprili, Mei, na miezi yote ya Kiangazi, ninataka
kucheza baseball. Muda wa miaka minne ya shule ya sekondari nilicheza
baseball. Baseball ni mchezo wa nchi ya Marekani kama mpira wa miguu
(soka) ni mchezo wa nchi ya Tanzania na Kenya.
Ili kucheza baseball, ni lazima kuwe na walau watu kumi. Tisa
kucheza kiwanjani au kinga, na walau mtu mmoja kucheza mpigaji. Moja wa
micheza wa shamba, ÔpitcherÕ, au mtu ambaye anarusha mpira wa baseball,
anarusha mpira wa baseball na mpigaji anajaribu kupiga mpira. Kama
mpigaji hawezi kupiga mpira mara tatu, mpigaji anatoka nje. Kama mpigaji
anaweza kupiga mpira, anakimbia kituo cha kwanza. Kama mpigaji anafika
kituo cha kwanza kabla ya mchezaji wa kinga hakudaka mpira, mpigaji
ameokoka Ôhe is safeÕ.
Katika Marekani, watu wa Marekani wanapenda baseball sana. Baba
na watoto wanaenda michezo ya baseball mara kwa mara. Karibu watoto wote
wa Marekani walicheza baseball au softball (mchezo kama baseball) walau
mkati mmoja katika maisha wangu. Mnamo Oktoba watu wa Marekani wengi
wanaangalia 'The World Series' katika televisheni. “The World Series” ni
mkasa maalum katika Marekani.
Nimeandika baseball kwa sababu ninapenda mchezo wa baseball sana.
Ninapenda mchezo wa baseball kwa sababu nilicheza baseball miaka kumi.
Nilicheza 'pitcher' na nilipenda kurusha kitonge cha baseball. Ninafikiri
kwamba nilirusha kitonge cha baseball kizuri muda wa miaka yangu ya
kucheza baseball. Muda wa miaka iliyopita ya schule ya sekondari, Chuo
Kikuu Cha Notre Dame ilinitaka kucheza baseball kwa Chuo Kikuu Cha Notre
Dame. Nilitaka kuwenda Notre Dame ili kucheza baseball sana, lakini
niliujeruhi mkono wangu na siliweza kucheza baseball tena. Sina kichaa,
pengine vitu vinajiri, lakini ninapenda baseball bado, na ninaangalia
baseball katika televisheni mara kwa mara.
Safari ya Amerika ya kusini
na Meredith Rapkin (Masika), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Mwaka tisini na nane, mwezi wa Februari, nilisafiri Amerika ya kusini,
nchi ya Uchile. Rafiki yangu anakaa katika mji wa santiago. Yeye ni
mwandishi wa habari kutoka Uchile, kwa njia ya internet. Jina lake ni
Dana. Katika Uchile nilisafiri pwani. Nilitembelea nyumba ya Pablo
Neruda. Yeye ni mshairi na alitoka Uchile. Pia, nilisafiri kusini ya
Uchile. Huko kuna kondoo wengi na milima mikubwa. Kuna maziwa mengi
pia.
Baada ya kusafiri katika Uchile wiki mbili, tulisafiri, dana na mimi,
Ubolivia kwa ndege. Tulifika La Paz na huko tulisikiliza musiki
na tulitembelea sehemu mbalimbali.Tulisafiri kichakani na jangwani pia
katika Ubolivia. Yulienda Ubolivia mnamo "carnaval", kwa hivyo tuliona
sherehe nyingi. Kuna utamaduni mmoja sipendi. Watoto wanarusha mabaluni
ya maji. Nilipata maji mara nyingi. Pia, tulisafiri katika ziwa Titicaca
na "kisiwa cha jua". Na baada ya kutembelea "kisiwa cha jua" tulienda
Uperu kwa gari la moshi. Tulitembelea Maachu Pichu, karibu na mji wa
Cuzco. Maachu Pichu iko juu ya mlima mmoja katika milima ya Andes. Mara
ya pili tulifika Santiago baada ya kusafiri mwezi moja.
Kuandika mashairi
na Tanaji Gillian (Asante), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Mimi ninapenda kuandika mashairi. Nilianza kuandika mashairi tangu
nilipokuwa na miaka misaba. Shairi langu la kwanza ni juu ya uhuru wa
Afrika ya Kusini, tenzi juu ya "Apartheid." Sasa ninaandika mashairi juu
ya mada nyingi. Mimi ni mwanachama wa "Assata." Assata ni kikundi cha
wanafunzi wanawake watano. Sote tunahudhuria Chuokikuu cha Penn. Majina
yetu ni Tanji, Jamarah, Sishu, Mecca na Ninah. Tulisoma mashairi yetu
hapa Penn na tulisoma katika Chuokikuu cha Jimbo la New Jersey pia.
Shabaha zetu ni kuwa na mayonesho na kurekudi "a C.D." Shairi langu bora
zaidi ni "The Real Hip-Hop" lakini mimi nina shairi la Kiswahili. Jina la
shairi ni "Umoja ni Nguvu"
Umoja ni Nguvu
Watoto wa Afrika
Karibu na mbali
Ni lazima turidi
Hadi asili ya uzazi
Children of Africa
Near and far
We must return
To the womb
Siku kabla ya ukoloni
Mateso ya wanaume wenye wivu
Ni lazima tushike
Uhuru wetu tena
Days before colonization,
The curse of jealous men
We must seize our freedom
Again
Jamaa zetu ni wengi
Ndugu zetu wanakaaMbr>
Katika nchi zote
duniani
Our family is numerous
Our siblings live
In every country
On Earth
Umoja ni nguvu
Tunahitajiana sisi kwa sisi
Kwa kukumbatiana
Tunarudia nyumbani
Unity is strength
We need each other
With our embrace
We return home
========================================
Madaktari bila Mipaka
na Camille Henry, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Madaktari Bila Mipaka
Doctors Without Borders
Medicine Sans Frontieres
Maaktari Bila Mipaka (MBM) ni shirika ambalo linawasaidia watu katika
hali ya hatari. Ni shirika kwa Ufaransa lakini linafanya kazi katika nchi
nyingi kwa duniani. MBM lipo Afrika, nchi za Asia, Amerika na Ulaya. Watu
kama madaktari, wawuguzi (nurses) na wafanyakazi wa afia wanajilotea
wakati wa misiba ambayo watu wanapata vita, njaa kuu, ugonjwa na
matetemeko ya ardhi. Wanasaidia watu na watoto ambao wanaelekea kupatwa
na cholera au ugonjwa wa kuambuzika ya Ebola , malaria, kutopata chakula
cha kutosha.
Watu ambao wanajitolea wapo pote katika Afrika kama nchi za
Tanzania na Kenya. Katika 1997, kulikuwa mvua kubwa katika Tanzania.
Halafu, watu wengi walipata ugonjwa na cholera katika sehemu za Kigoma
(katika magharibi na kaskazini), Dar-Es-Salaam, Mtwara (katika mashariki
ya kusini) na Zanzibar. Waliwapa dawa wagonjwa, walisaidia kusafisha
maji ya kunwya na waliwafundisha wafanyakazi wa afia wa Tanzania. Sasa
katika Kigoma pia wanawasaidia katika hospitali wakimbizi wa Zaire na
Rwanda ambao wametoroka vitu na mauwaji katika nchi zao.
Katika nyumba za wamaskini wa Nairobi (kama Mathare, Dandora,
Kibera na Pumwani) wafanyakazi wa MBM wanafanya maazimio ya afiya ili
wapigane na UKIMWI pamoja na Wakenya. Katika sehemu za Laikipia na Njoro
na Likoni, madaktari wa MBM wanafanya kazi na watu elfu kumi na tatu, mia
tano, na waliipiga chanja ya surua, walitoa dawa na kadhalika.
Ninayapenda mashirika kama Maktari Bila Mipaka kwa sababu yanawasaidia
watu maskini wo wote, bila ujira na bila ya ubaguzi.
shirika - organisation
hatari - danger/peril/risk
wawuguzi - nurses
wafanyakazi wa afia - health workers
kujitolea - to volunteer
misiba - emergencies
vita - war
njaa kuu - famine
ugonjwa - disease
matetemeko ya ardhi - earthquakes
kutopata chakula cha kutosha - malnutrition.
wakimbizi - refugees
wanatoroka (Kutoroka) - to flee
mauwaji - killings
maazimio ya afiya - health programmes
kupigana na - fight against
UKIMWI - AIDS (Upungufa wa Kinga Mwilini)
ujira - pay, salary
ubaguzi - discrimination
==========================================
Kuchonga
na Mathew Simon (Bakari), mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
Mimi ni mchongaji. Kuchonga ni kufanya vitu kwa miti.
Sijafundishwa vipi kufanya sanaa, lakini ninajaribu kujifundisha.
Ninapenda kufanya vitu kwa kutumia miti. Nimefanya sanamu za nyuso na
vichwa na mwili wote. Pia nimefanya ngao na ngoma ndogo.
Kufanya vitu hivi ninatumia vyombo vya mkono. Vyombo vingine
nilijinunulia. Nina visu vikali na vyombo vingine vikali ambavyo
ninatumia. Pia nimefanya vyombo vingine au nimebadili vingine ili
vifanye vizuri zaidi. Vyombo vingine nilipewa. Baba yangu alinipa panga
lake. Alilitumia kukata miwa. Kwasababu sasa hakai karibu na miwa na
hahitaji kukata miwa, Baba yangu alinipa panga yake. Nilifanya likali na
ninalitumia kuchonga.
Ninatumia panga kuondoa maganda ya miti na kukata vipande
vikubwa. Ninatumia visu kukata vipande vidogo. Baadhi ya wakati
ninafanya picha kabla ya kuchonga.
Baada ya kufany umbo, ninatumia msasa. Msasa ni karatasi ya
mchanga. Msasa huu uondoa vipande vidogo vidogo. Baada ya kutumia msasa
ninamaliza kwa kutumia polish kupaka rangi mti.
Baadhi ya wakati nimepoteza vitu ambavyo nimefanya. Baadhi ya
wakati ninawapa vitu rafiki yangu. Kuna vitu viwili nilivyofanya lakini
havijamalizika. Vitu viwili ni sanaa ya vichwa.
MCHEZO WA MANENO
Maneno gani yenye herufi nne au zaidi unaweza kuyatoa kwenye neno
TULIKWENDA?
Niandikie.