Nyimbo hizi zimeimbwa katika darasa la Kiswahili la televsheni kwa ajili ya shule za Philadelphia.

      Mwalimu wa darasa: Dr. Alwiya S. Omar

      1. Jambo

      Sikiliza

      Jambo, Jambo sana!

      Habari gani? Nzuri sana.

      Wanafunzi, wakaribishwa.

      Darasani kwetu, hakuna matata.

      Walimu wetu, Hakuna matata.

      Na wanafunzi wetu , Hakuna matata.

      Shuleni kwetu, Hakuna matata.

      2. Nambari

      Sikiliza

      Moja, mbili, tatu

      Nne, tano, sita

      Saba, nane, tisa

      Kumi ni ya mwisho

      Sasa tunaka kuhesabu tena

      Kwahivyo tuanze moja mpaka kumi

      3. Kichwa, vidole

      Sikiliza

      Kichwa, vidole, mabega magoti

      Mabega, magoti, mabega, magoti.

      Kichwa, vidole, mabega, magoti.

      Macho, pua, masikio.

      4. Wimbo wa Taifa wa Tanzania

      Sikiliza

      Mungu ibariki Afrika
      Wabariki viongozi wake
      Hekima, umoja na amani
      Hizi ni ngao zetu
      Afrika na watu wake
      Ibariki. Afrika
      Ibariki. Afrika
      Tubariki watoto wa Afrika

      Mungu ibariki Tanzania
      Dumisha uhuru na umoja
      Wake kwa waume na watoto
      Mungu ibariki
      Tanzania na watu wake
      Ibariki. Tanzania
      Ibariki. Tanzania
      Tubariki watoto wa Tanzania

      ========Waimbaji=========

      Khadija Shariff, Talha Omar, Idarousse Shariff, na Mustafa Shariff

      5. Wimbo wa Taifa wa Kenya

      Sikiliza

      Ee Mungu nguvu yetu
      Ilete baraka kwetu
      Haki iwe ngao na mlinzi
      Na tukae na undungu
      Amani na uhuru
      Raha tupate na ustawi

      =======mwimbaji na mpigaji kifilimbi===========
      Mpigaji kifilimbi: James Wilson
      Mwimbaji" Kabuiya Kimani

      Last modified: December 16th, 1997

      Alwiya S. Omar, asomar@babel.ling.upenn.edu
      African Language Coordinator

      Nenda ukurasa waTuzungumze Kiswahili

      Course Outline

      Kiswahili at Penn